10 Aprili 2022 - 13:38
Wafaransa wanapiga kura katika uchaguzi wa rais

Wafaransa leo wanapiga kura katika duru ya kwanza kumchagua rais, huku kukitabiriwa mchuano mkali kati ya Rais Emmanuel Macron na mwanasiasa mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia Marine Le Pen.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa mbili asubuhi saa za Paris, lakini raia wa Ufaransa wanaoishi nje ya nchi na wale wanaoshi katika visiwa vinavyomilikiwa na nchi hiyo, wamekuwa wakipiga kura tangu Jumamosi

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kufahamika baadaye leo Jumapili usiku, huku wadadisi wa siasa wakisema Macron atatofautiana na mpinzani wake Le Pen kwa asilimia ndogo na hivyo wawili hao watachuana katika duru ya pili Aprili 24. 

Ili kumpata mshindi katika duru ya kwanza, mgombea anapaswa kupata asilimia 50 ya kura zote. 

Mbali na Macron na Le Pen, kuna wagombea wengine 10 wanaowania nafasi ya kuongoza taifa hilo la Ulaya, akiwemo mwanasiasa mkongwe mwenye siasa za mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon, ambaye huenda akamaliza katika nafasi ya tatu. 

Kuna wasiwasi kuwa, kuna idadi kubwa ya wapiga kura hawatajitokeza katika zoezi la upigaji kura leo.

342/